Uchumi wa nchi ya Japan umeimarika tena baada ya michuano ya Olimpiki zaidi ya ilivyotegemewa baada kudhoofishwa na janga la UVIKO-19.
Tathmini rasmi zinaonyesha Taifa hilo la tatu kiuchumi duniani limekua mara mbili zaidi ya ilivyotazamiwa kwa miezi ya Aprili mpaka Juni.
Wakati huo huo tathmini rasmi zinaonyesha kuwa ukuaji wa uchumi wa jirani yao, China umeanza kudhoofika.
Nchi nyingi duniani zimeathiriwa na janga la UVIKO-19, michezo ya Olimpiki imeisaidia Japan kupambana na janga hilo na kuurudisha uchumi wake.