Ubaguzi wa rangi wamliza Vinicius

0
529

Winga wa Brazil na Real Madrid,Vinicius Jr (23) amejikuta akitokwa machozi wakati akijibu swali kuhusu ubaguzi wa rangi anaokumbana nao katika maisha yake ya soka nchini Hispania.

Vinicius amesema mara nyingi huingia uwanjani akijikita zaidi kwenye kucheza mpira, lakini sio mara zote anafanikiwa na kwamba vitendo vya ubaguzi kutoka kwa mashabiki humtoa mchezoni.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa hatochutama na kuondoka Real Madrid na Hispani kwa shinikizo la mashabiki na kuacha vitendo vya ubaguzi vishinde.

Msimu uliopita kulikuwa na matukio 10 ya ubaguzi dhidi yake.

Kikosi cha Brazil kipo nchini Hispania ambapo kitacheza mchezo wa kirafiki katika dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid, mchezo ambao ni sehemu ya kampeni ya kupiga vita ubaguzi wa rangi inayokwenda kwa jina ‘One skin.’