Tume ya Uchaguzi Uganda yasisitiza uchaguzi ulikuwa huru

0
180

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Uganda imetupilia mbali madai yanayotolewa na baadhi ya watu kuwa, kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu wakati wa uchaguzi wa Rais na Wabunge uliofanyika tarehe 14 mwezi huu.

Maafisa wa Tume hiyo wamesema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.na ulifanyika katika mazingira ya amani na utulivu.

Wamesisitiza kuwa, changamoto zote zilizojitokeza kabla, wakati na baada ya uchaguzi huo zilishughulikiwa kwa haraka.

Tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Uganda imemtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi wa kiti cha urais kwa kipindi kingine cha sita.

Museveni ametangazwa mshindi baada ya kupata kura milioni 5.85 ambazo ni sawa na asilimia 58.64 ya kura zote zilizopigwa.

Mpinzani wa karibu wa Museveni katika kinyang’anyiro cha Urais alikuwa Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, ambaye amepata kura milioni 3.48 sawa na asilimia 34.83 ya kura zote zilizopigwa.

Rais Yoweri Museveni tayari ameiongoza Uganda kwa takribani miaka 35.
.