Tanzania yakipigia chapuo kiswahili Msumbiji

0
177

Rais Samia Suluhu Hassan ameiomba serikali ya Msumbiji kuandaa mipango itakayowezesha lugha ya kiswahili kuingizwa katika mifumo ya elimu ya nchini humo.

Rais Samia ametoa ombi hilo nchini Msumbiji alipokuwa akihutubia kongamano la 12 la chama cha
tawala cha nchi hiyo cha Mozambican Liberation Front (FRELIMO).

Amesema lugha ya kiswaiili inaweza kutumika Msumbiji katika kuwaunganisha wananchi, hasa baada ya lugha hiyo kutambuliwa kimataifa.

Rais Samia amesema kwa miaka mingi iliyopita lugha ya kiswahili iliwasaidia wapigania Uhuru Barani Afrika kuwasiliana, hivyo kwa sasa ina uwezo wa kuwaunganisha waafrika wote.

Kongamano hilo la 12 la chama cha FRELIMO linafanyika wakati chama hicho kikiwa kimetimiza miaka 60 tangu kuasisiwa kwake June 25 mwaka 1962 mkoani Dar es Salaam, Tanzania.

Lengo la kongamano hilo la 12 la chama cha FRELIMO ni kuweka mikakati imara kwa ajili ya kukiendeleza chama hicho pamoja kuisimamia serikali.