Rais Samia Suluhu Hassan ambaye yupo Davos, Uswisi amekutana na wawekezaji katika mkutano uliokuwa na lengo la kuitangaza Tanzania katika sekta ya mbalimbali za uwekezaji.
Wakati wa mkutano huo Rais Samia akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na wawekezaji, wametazama picha za video zinazoitangaza Tanzania katika sekta mbalimbali.
Dkt. Samia ametumia mkutano huo kuwaeleza viongozi hao pamoja na wawekezaji kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana Tanzania.
Katika hatua nyingine, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uswisi, Alain Berset katika ukumbi wa mikutano wa Congress.