Tanzania yaikaribisha klabu ya Fenerbehche

0
136

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, ametembelea moja ya klabu kongwe na mashuhuri duniani Fenerbehche ya Uturuki na kukubaliana kushirikiana katika maeneo ya mafunzo, kambi na ujenzi wa shule za michezo.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika nchini Uturuki na kuongozwa na mjumbe wa bodi ya klabu hiyo anayeshughulikia masuala ya kimataifa, Bekir Irdem, Waziri Mchengerwa pia ameishukuru klabu hiyo kwa kuwahi kuwa na mchezaji kutoka Tanzania, Mbwana Sammatta na kuikaribisha klabu hiyo kuweka kambi ya msimu mpya mwaka 2023 nchini Tanzania.

“Leo tu baadae tutakuwa na kikao cha bodi na nitawasilisha mapendekezo haya ili tuweze kuanza ushirikiano wetu mara moja.” ameahidi Irdem

Katika ziara hiyo, Waziri Mchengerwa amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Luteni Jenerali Yacoub Mohammed na Katibu Mkuu wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi.