Takribani watu mia moja kumi na watano hawajulikani walipo

0
417

Takribani watu mia moja kumi na watano hawajulikani walipo na wengine kuhofiwa kuzama baada ya boti iliyobeba watu mia mbili na hamsini kuzama umbali wa kilomita nane kutoka pwani ya LIBYA.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na msemaji wa Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR CHARLIE YAXLEY, tukio la kuzama kwa boti hiyo ni baya zaidi kutokea kwa mwaka  huu, ambapo idadi kubwa ya watu waliokuwa katika boti hiyo wanatoka mataifa mbalimbali ya Afrika na yale ya kiarabu.

Hata hivyo watu mia moja, thelathini na wanne wameokolewa na baadhi yao kutambuliwa, baada ya wavuvi kushirikiana na vikosi vya uokoaji kufanikisha zoezi la awali la uokoaji baada ya kuzama kwa boti hiyo.

Msemaji huyo wa UNHCR ameongeza kuwa watu hao walio okolewa watapelekwa katika kambi maalumu nchini LIBYA kabla ya kufanyika kwa utaratibu mwingie wa kutoa huduma kwa watu hao waliokuwa wakisafiri kutoka Libya kutelekea mataifa mbalimbali ya Ulaya.