Syria yashutumiwa kutumia silaha za kemikali

0
533

Balozi wa Marekani nchini Syria, – Jim Jeffrey amesema kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwa vikosi vya serikali ya Syria vinajiandaa kutumia silaha za kemikali katika mji wa Idlib.

Kauli ya Jeffrey inaelekea kufanana na ile ya serikali ya Marekani iliyotolewa mwanzoni mwa wiki hii ambayo ilionya kujibu shambulio lolote litakalofanywa na vikosi vya serikali ya Syria ama washirika wake kwa kutumia silaha za kemikali.

Hata hivyo serikali ya Syria imekanusha vikosi vyake kujiandaa kutumia silaha hizo za kemikali na pia kuzitumia katika miji mbalimbali katika siku za nyuma kama inavyodaiwa na watu mbalimbali.

Licha ya Syria kukanusha tuhuma hizo, wataalam kutoka Umoja wa Mataifa pamoja na Shirika la kuzuia matumizi ya silaha za kemikali wamesema kuwa wana ushahidi kuwa vikosi hivyo vya Syria vilihusika na shambulio la kutumia silaha za kemikali katika mji Idlib unaoshikiliwa na waasi mwezi Aprili mwaka 2017 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu Themanini.