Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Sudan vimezima jaribio la mapinduzi ya kijeshi.
Maafisa wa Serikali ya Sudan wamesema, watu waliohusika katika jaribio hilo la mapinduzi walijaribu kuchukua udhibiti wa vituo vya Taifa vya redio na televisheni katika mji wa Omdurman, lakini walidhibitiwa nguvu na vikosi hiyyo vya ulinzi na usalama.
Serikali ya Sudan bado haijatangaza watu waliohusika na jaribio hilo la mapinduzi ya kijeshi, ingawa wahusika kadhaa wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa.
Vifaru na wanajeshi kadhaa wameonekana kufanya doria katika miji mbalimbali nchini humo kufuatia jaribio hilo la mapinduzi ya kijeshi lililoshindwa.