Sudan na Libya kujadiliwa kwa dharula na AU

0
375

Mkutano wa dharula wa Umoja wa Afrika (AU) wenye lengo la kujadili hali ya Sudan na Libya unafanyika hii leo nchini Misri.

Rais Abdel Fattah Al – Sisi wa Misri, ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa  AU ndiye anayeongoza mkutano huo  ambao kwa kiasi kikubwa  unajadili hali ya Sudan ambapo  Omar Al-Bashir aliyekua Rais wa nchi hiyo aliondolewa madarakani kufuatia maandamno ya wiki kadhaa yaliyofanywa na Raia.

 Kuhusu hali ya Libya, viongozi hao wa nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika  wanajadili mapigano yanayoendelea hivi sasa baina ya vikosi vya serikali na vile vinavyomuunga mkono mbabe wa kivita nchini humo Jenerali Khalifa Haftar.

Wakuu wa nchi wanaohudhuria mkutano huo wanatoka Chad, Rwanda, Congo-Brazzaville, Somalia, Djibouti  na Afrika Kusini.