Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Elibariki Bajuta ambaye anahudhuria vikao mbalimbali vya Haki za Binadamu Geneva, Uswisi ametembelea Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu za Tanzania Geneva na kutoa Elimu kuhusu uhifadhi wa wanyama pori.
Bajuta ametoa wasilisho kwa watumishi wa Ofisi hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya Maliasili ya Taifa na namna zinavyo hifadhiwa.
Bajuta amepata fursa ya kuelezea masuala mbalimbali yanayohusu Maliasili zilizopo hapa nchini.