Sherehe za siku ya Afghanistan zasitishwa

0
199

Serikali ya Afghanistan imesitisha sherehe za siku ya Taifa hilo, baada ya watu Sitini na Watatu kuuawa katika shambulio la kujitoa mhanga lililotokea katika sherehe za harusi mjini Kabul.

Sherehe za kutimiza miaka Mia Moja ya uhuru wa Afghanistan zinafanyika kimya kimya,  ili kuepuka mikusanyiko ya watu, jambo linaloweza kuwafanya washambuliaji kutumia mwanya huo kutekeleza shambulio jingine.

Wakati huohuo,  zoezi la kuwazika watu waliouwa katika shambulio hilo lililoanza jana linaendelea  hii leo mjini Kabul, huku ndugu na jamaa za watu waliokuwa kwenye sherehe za harusi wakiendelea kuwatambua ndugu zao walioathiriwa na shambulio hilo.

Wanamgambo wa kikundi cha IS wanadai kuhusika na shambulio hilo, huku awali Wanamgambo wengine wa kikundi cha Taliban wakiwa wametuhumiwa kuhusika, lakini baadaye wakakanusha.