Watu 230 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya wapiganaji wa kikundi cha Oromo Liberation Army (OLA) kuwashambulia wananchi wa jamii ya Tole katika kijiji kimoja kwenye mkoa wa Oromo nchini Ethiopia.
Shambulio hilo limeelezwa kuwa ni baya zaidi kuwahi kutokda nchini humo na kwamba linaweza kuchochea machafuko ya kikabila katika maeneo mengine kwenye mkoa huo.
Kundi la Oromo Liberation Army limekanusha kuhusika na shambulio hilo na kudai kwamba mauaji hayo yametekelezwa na makundi yanayoiunga mkono serikali ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Dkt. Abiy Ahmed.