Serikali yathibitisha madai ya mwanafunzi

0
228

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema ni kweli mwanafunzi wa shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primary, Iptisum Slim pamoja na wanafunzi wengine sita walibadilishiwa namba ya mtihani. katika mtihani wa taifa wa darasa la saba uĺiofanyika tarehe 5 na 6 mwezi huu.

Profesa Mkenda amebainisha hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Dar es salaam.

Amesema uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa mwanafunzi huyo pamoja na wanafunzi wengine sita walibadilishiwa namba ya mtihani katika mtihani wa Taifa wa darasa la saba.

Kufuatia tukio hilo Profesa Mkenda ameagiza watumishi waliohusika na udanganyifu katika mtihani wa darasa la saba kwenye shule hiyo ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primary kuchukuliwa hatua.

Pia ameifunga shule hiyo kuwa kituo cha kufanyia mtihani kwa muda usiojulikana.