Serikali ya Hispania kupokea wahamiaji na wakimbizi waliozuiliwa katika bahari ya Mediterranean.

0
2287

Serikali ya Hispania imesema itapokea boti ya uokoaji iliyokua imebeba zaidi ya wahamiaji na wakimbizi 600 na kuzuiliwa katika bahari ya Mediterranean na Mamlaka ya usafiri wa majini ya Italia.

Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sanchez aliyeingia madarakani wiki iliyopita ametoa agizo kwa mamlaka husika kufikisha boti hiyo katika bandari ya Valencia.

Amesema ni jukumu la kila mmoja kutoa msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi ili kuishi katika mazingira salama ikiwa ni haki yao ya msingi.

Habari zinasema kuwa boti hiyo imebeba watu 130 wakiwemo watoto 123.

 

Herieth Shija

11 Juni 2018