Semenya ajiamini kurejea kwenye riadha jinsi alivyo

0
174

Mawakili wa bingwa wa Olimpiki mara mbili, Caster Semenya wanasema mteja wao “anajisikia utulivu na kujiamini” kabla ya kusikilizwa kwa kesi inayohusu kama atatakiwa kupunguza viwango vyake vya homoni za kiume (testosterone) kabla ya kushiriki mashindano ya riadha kama mwanamke au la.

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu iliyoko Strasbourg, Ufaransa, inasikiliza kesi hiyo leo kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho katika tarehe itakayotajwa baadaye.

“Nina matumaini kwamba uamuzi wa mahakama utaonesha njia itakayozingatia haki za binadamu za wanariadha wote kulindwa sawasawa, na kuhamasisha wasichana wote kujikubali katika utofauti wowote waliozaliwa nao,” Semenya amesema katika taarifa iliyotolewa. na wanasheria wake.

Semenya, 33, alizaliwa akiwa na tofauti za ukuaji wa kijinsia (DSD), kundi adimu ambalo mtoto anazaliwa akiwa na mchanganyiko wa homoni au jeni zenye sifa za kiume na za kike.

Alizuiwa na bodi inayosimamia riadha duniani kushiriki mashindano ya mbio za wanawake labda kama atatumia dawa za kupunguza homoni za kiume alizozaliwa nazo za testosterone.

Mwanariadha huyo, raia wa Afrika Kusini anapinga hatua hiyo akiamini bodi hiyo ya kimataifa inayosimamia riadha imeonyesha ubaguzi dhidi ya wanariadha kulingana hali zao ambazo hawakujiombea kutoka kwa muumba wao.

Lakini Bodi hiyo ya Riadha ya Duniani inasema kanuni zake zake kuhusu wenye DSD “ni njia muhimu yenye kuleta usawa na haki katika mashindano ya riadha kwa wanawake.”

Kama wewe ungekuwa jaji wa hii kesi ungeamua nini?

Chanzo: BBC