Bunge la nchini Scotland limepigia kura ya siri mswada wa utolewaji wa taulo za wanawake (sanitary pads & tampons) bure, mswada ambao umepata kura nyingi.
Pedi hizo zitatolewa bure katika maeneo ya wazi kwa umma na jumuiya mbalimbali, ikiwemo vyuoni na shuleni, na hivyo viongozi kuombwa kuhakikisha wanafunzi wao wanapata vifaa hivi.
Monica Lennon, mbunge aliyepeleka mswada huu kwa mara ya kwanza mwaka jana kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema, “Siku ya kujivunia kwa Scotland na ishara kwa ulimwengu kuwa upatikanaji wa bure wa vifaa vya hedhi unawezekana.”
Kupitishwa kwa mswada huo kumeifanya Scoatland kuwa nchi ya kwanza duniani kutoa pedi bure.