Msemaji wa Ikulu ya Marekani ,Sarah Sanders kuachia nafasi hiyo mwishoni mwa mwezi huu.
Akitangaza kuondoka kwa msemaji huyo, Rais Donald Trump wa Marekani katika ukurasa wake wa Tweeter amesema Sanders alikuwa ni mtu mwenye kipaji cha tofauti na amefanya kazi nzuri ya kukumbukwa.
Sanders amefanya kazi katika Ikulu ya Marekani kwa muda wa miaka mitatu na nusu, na bado Rais Trump hajatangaza mrithi wa nafasi hiyo.