Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Uturuki amewasilisha ombi la hati ya kukamatwa kwa viongozi wawili wa ngazi za juu nchini Saudi Arabia kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha mwandishi wa habari maarufu wa Saudi Arabia, – Jamal Kashoggi.
Miongoni mwa watu wanaotuhumiwa kuhusika na kifo cha Kashoggi, na ambaye ameorodheshwa katika hati hiyo ya kukamatwa ni aliyekuwa mkuu wa masuala ya Kiintelijensia wa Saudi Arabia, Ahmed Al Siri na mshauri wa utawala wa kifalme wa nchi hiyo Saud Al Kathani.
Watu hao wanatuhumiwa kupanga mauaji ya Kashoggi mwezi Oktoba mwaka huu mjini Istanbul nchini Uturuki kwenye ubalozi mdogo wa Saudi Arabia.