Rais wa zamani wa Ivory Coast aachiwa huru

0
923

Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai Icc imemuachilia huru aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo.

Majaji wa mahakama hiyo wamesema hana kesi ya kujibu kwa sababu upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha makosa dhidi yake na kuamrisha kuachiwa huru mara moja.

Gbagbo alishtakiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya raia wa Ivory Coast kufuatia ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi uliokuwa na mzozo wa 2010 zilizopelekea takriban watu 3000 kuuwawa na wengine 500,000 kuachwa bila makazi .

Gbagbo alikamatwa  mwaka 2011 na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa Un pamoja na wale wanaoungwa mkono na UfaransA waliokuwa wakimuunga mkono mpianzani wake Alassane OuattarA.

Wafuasi wa Gbagbo wameonekana wakisherehekea katika maeneo mbalimbali  kufuatia kuachiwa huru kwa kiongozi huyo.