Rais wa Ufaransa akutwa na Corona

0
186

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amebainika kuambukizwa virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo.

Kabla ya kufanyiwa vipimo hivyo, Rais Macron mwenye umri wa miaka 42 alikuwa na dalili mbalimbali za maambukizi ya virusi hivyo, ambapo maafisa wa afya wanafanya uchunguzi kubaini sehemu ambayo Rais huyo alipata maambukizi hayo.

Tayari Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex pamoja na Spika wa Bunge la nchi hiyo Richard Ferrand wamejiweka katika karantini binafsi ili kubaini kama nao wamepata maambukizi hayo kwa kuwa wanafanya kazi kwa ukaribu na Rais Macron.

Mwanzoni mwa wiki hii Ufaransa ilipitisha sheria ya kuzuia mikusanyiko ya watu hasa nyakati za usiku ikiwa ni hatua ya kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.