Rais wa Mali anusurika kuuawa

0
255

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais wa Mali imesema Rais Assimi Goïta wa nchi hiyo yuko salama baada kutokea kwa jaribio la shambulio la kisu katika msikiti mmoja uliopo kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Bamako.

Jaribio hilo limetokea katika msikiti wa Grande ambapo Kanali Goïta aliungana na waumini wengine wa dini ya Kiislam kuswali sala ya Eid Al Adha.  
                               
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa, watu wawili mmoja akiwa na kisu ndio waliofanya jaribio la kumshambulia Rais Goïta.

Taarifa hiyo imesema tayari watu hao wawili wamekamatwa na Kanali Goïta amepelekwa katika kambi ya jeshi iliyo karibu na mji wa Bamako.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Mali imesema shambulilio hilo lililenga kumdhuru Rais Goïta.

Kanali Goïta anafahamika kama miongoni mwa watu hatari, na katika kipindi cha mwaka mmoja amefanya majaribio mawili ya kijeshi.