Rais wa Iran, Ebrahim Raisi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo IHossein Amir- Abdollahian wamethibitika kufariki dunia baada ya helkopta waliyokuwa wakisafiria kuanguka wakati wakielekea katika mji wa Tabriz uliopo Kaskazini Magharibi mwa Iran.
Chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa kuwa ni hali mbaya ya hewa ukiwepo ukungu katika eneo ilipotokea ajali hiyo, hali iliyoifanya helikopta hiyo kupata wakati mgumu kutua.
Helikopta hiyo ni miongoni mwa helikopta tatu zilzokuwa katika msafara huo, ambapo mbili zilitua salama.
Kabla ya ajali hiyo kutokea, Rais huyo wa Iran alishiriki katika ufunguzi wa mabwawa mawili karibu na mpaka wa Iran na Azerbaijan.
Raisi alichaguliwa kuwa Rais wa Iran mwaka 2021.