Rais Samia kukutana na Papa Francis

0
529

Rais Samia Suluhu Hassan leo Februari 12, 2024 anafanya ziara ya kikazi Vatican ambapo pamoja na mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Francis.

Baada ya mazungumzo hayo, Rais Samia atakutana na Kadinali Pietro Parolin ambaye ni Msaidizi Mkuu wa Papa Francis kwenye Serikali ya Vatican pamoja na Askofu Paul Gallagher, Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa wa Vatican.

Rais Samia anafanya ziara hiyo Vatican kufuatia mwaliko wa Papa Francis na katika ziara hiyo amefuatana na Wawakilishi wa waumini wa Kanisa Katoliki kutoka Tanzania.

Il Presidente della Repubblica Sergio Mattarella incontra Papa Francesco