Rais Samia awasili Uturuki

0
427

Rais Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ankara Esenboga nchini Uturuki leo Aprili 17, 2024 kwa ajili ya ziara.

Rais Samia amefanya mazungumzo na Waziri wa Familia na Huduma za Jamii wa Uturuki, Mahinur Ozdemir Goktas mara baada ya kuwasili katika uwanja huo wa ndege.

Akiwa nchini humo, Dkt. Samia atatunukiwa shahada ya udaktari wa heshima katika uchumi na Chuo Kikuu cha Ankara kabla ya kukutana na mwenyeji wake, Rais Recep Erdogan.