Umoja wa Watemi wa Kisukuma kwa kushirikiana na Umoja wa Machifu Tanzania umemsimika Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mkuu wa Machifu Tanzania na kumpa jina la Hangaya, lenye maana ya Nyota inayong’aa asubuhi.
Rais Samia Suluhu Hassan amesimikwa kuwa mkuu wa Machifu wakati wa tamasha la Utamaduni wa Mtanzania ambalo linafikia kilele chake hii leo huko wilayani Magu mkoani Mwanza
Katibu wa Umoja wa Machifu wa Kisukuma, Mtemi Aaron Mikomangwa amesema wamemsimima Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mkuu wa Machifu Tanzania na jina hilo la Hangaya ikiwa ni kutambua mchango wa Serikali yake katika kuthamini na kusimamia utu wa wanyonge pamoja na utamaduni wa Mtanzania.
Lengo la tamasha hilo la Utamaduni wa Mtanzania lililoanza jana, ni kudumisha, kurithisha na kuutangaza utamaduni wa makabila ya Tanzania.