Rais Samia Suluhu Hassan, leo Mei 31 2024 ameanza ziara rasmi Korea Kusini kwa mwaliko wa Rais Yoon Suk Yeol wa nchi hiyo.
Akiwa nchini humo Rais Samia atashiriki mkutano baina ya viongozi wa Afrika na Korea Kusini utakaofanyika Juni 4 hadi 5, 2024.
Wakati wa ziara hiyo, Tanzania na Korea Kusini zitatia saini makubaliano mapya ya mkopo wa riba nafuu wa dola Bilioni 2.5 kwa ajili ya miradi ya kimaendeleo kwa takribani miaka mitano ambayo ni 2024-2028.
Ushirikiano kati ya Tanzania na Korea Kusini uliasisiwa mwaka 1992 ambapo kati ya mafanikio ya ushirikiano huo ni pamoja na ujenzi wa daraja la Tanzanite lililopo mkoani Dar es Salaam.
✍️ @fredricknwaka
Seoul, Korea Kusini.