Rais Ruto amteua Kenyatta

0
192

Kenyatta mjumbe wa amani mgogoro wa Tigray

Rais wa Kenya William Ruto amemteua Rais mstaafu wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta kuwa Mjumbe wa amani katika mgogoro wa jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia.

Uteuzi huo umefanyika siku chache baada ya Kenyatta kustaafu uongozi wa nchi hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ulaya, Joseph Borrell amekaribisha uteuzi huo na kuitaja Kenya kama mshirika muhimu katika pembe ya Afrika.