Rais Museveni kusafiri kwa Treni Kenya

0
537

Rais Yoweri Museveni wa Uganda anatarajiwa kusafiri kwa kutumia treni ya kisasa kutoka  kwenye mji wa Mombasa kwenda mji mkuu wa Kenya, – Nairobi na kuwa kiongozi wa kwanza kutoka nje ya Kenya kusafiri kwa treni hiyo.

Katika safari hiyo Rais Museveni ataongozana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, viongozi ambao katika mazungumzo yao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano baina ya Uganda na Kenya.

Rais Museveni ambaye yuko nchini Kenya  kwa ziara ya kikazi,  atatumia muda wa saa Nne tu kusafiri umbali wa Kilomita  480 kutoka mji huo wa Mombasa kwenda Nairobi.

Katika mazungumzo yake na Rais Kenyatta, Rais Museveni  amesema kuwa reli hiyo ya kisasa nchini Kenya ambayo ujenzi wake umegharimu Dola Bilioni 3.2 za Kimarekani, itasaidia kurahisisha usafirishaji mizigo kutoka katika bandari ya Mombasa kwenda kwenye mji mkuu wa Uganda, – Kampala.