Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameagiza kukamatwa kwa watu wote wanaosambaza uvumi kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia.
Amesema amechoshwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kumsema vibaya yeye pamoja na familia yake.
Akitoa agizo hilo Rais Museveni amesema kuwa, baadhi ya mitandao ya kijamii nchini Uganda imekuwa kero hivyo kunahitajika kuangaliwa upya kwa kanuni na sheria za uendeshaji wa baadhi ya mitandao hiyo.
Katika siku hivi karibuni baadhi ya mitandao ya kijamii nchini Uganda imekuwa ikiandika habari za uzushi kuhusu afya ya Rais Museveni pamoja na mtoto wake mkubwa wa kiume.