Rais Mstaafu wa Kenya, Daniel Moi afariki dunia

0
460
Daniek arap Moi alikuwa Rais wa Kenya kuanzia 1978 hadi 2002.

Rais wa Pili wa Kenya, Daniel Toroitich arap Moi amefariki dunia leo February 4, majira ya saa 11 asubuhi katika Hospitali ya Nairobi.

Rais Uhuru Kenyatta, ametangaza leo asubuhi katika salamu zake za pole kwa familia na taifa kwa ujumla.

Moi alizaliwa Septemba 2, 1924 na aliliongoza taifa hilo kwa miaka 24 tangu 1978 alipotwaa madaraka kufuatia kifo cha Rais wa Kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta, hadi 2002 alipompisha Mwai Kibaki.

Taifa hilo limetangaza siku za maombolezo kuanzia leo Jumanne hadi kiongozi huyo atakapozikwa.

Moi ambaye ni baba wa watoto nane alimuoa Lena Moi, lakini wawili hao waliachana mwaka 1979, na mkewe huyo alifariki dunia mwaka 2004.