Rais aliyepinduliwa Niger aomba msaada wa Marekani

0
365

Rais wa Niger aliyepinduliwa, Mohamed Bazoum ameiomba Marekani na jumuiya ya kimataifa kusaidia kurejesha utawala wa kiraia nchini humo kufuatia mapinduzi ya kijeshi juma lililopita.

Katika chapisho lake alilosema anaandika akiwa kama mateka amesema huenda ukanda wa Afrika Magharibi ukawa chini ya ushawishi wa Urusi kupitia Wagner Group, kundi ambalo tayari lipo nchi jirani.

Baadhi ya nchi za ukanda huo zimetishia kuwa zitatekeleza hatua za kijeshi endapo nchi nyingine ya Afrika au Magharibi itavamia Niger kwa madai ya kurejesha utawala wa Bazoum.

Tayari Niger imewaondoa nchini humo mabalozi wa nchi nne ambazo ni Ufaransa, Marekani, Nigeria na Togo.

Niger ni moja ya nchi maskini zaidi duniani licha ya kuwa mzalishaji mkubwa wa uranium inayotumika kuzalisha umeme kwenye vinu vya nyuklia nchini Ufaransa pamoja na kutumika kwenye utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki.