Putin avunja ukimya kifo cha Yevgeny Prigozhin

0
471

Rais wa Urusi, Vladimir Putin amevunja ukimya kufuatia taarifa za kifo cha kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin, baada ya ndege aliyokuwa akisafiria yeye na watu wengine tisa kutoka Moscow kwenye St. Peterburg kuanguka.

Putin amesema kuwa Prigozhin alikuwa ni mtu mwenye kipaji ambaye “alifanya makosa makubwa katika maisha.”

Aidha, Rais Putin ametuma rambirambi kwa familia za watu wote 10 waliofariki katika ajali hiyo.

Hata hivyo, kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu hasa chanzo cha ajali hiyo na kama ni kweli Yevgeny Prigozhin alikuwemo kwenye ndege hiyo kama inavyoonekana kwenye orodha ya abiria.

Kufuatia ajali hiyo, Marekani imesema inaamini kuwa kiongozi huyo aliuawa.

Wengi wenye mashaka na kifo hicho wanahusisha na jaribio la mapinduzi alilolifanya Juni mwaka huu, wengi wakimuona sawa na “mtu aliyefariki anatembea.”