Polisi Kenya watumia mabomu ya machozi kudhibiti corona

0
718

Jeshi la polisi nchini Kenya usiku wa kuamkia leo limelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wananchi ambao wanapinga agizo la serikali linalowataka kutokuwa nje kuanzia saa moja usiku ili kudhibiti maambukizi zaidi ya virusi vya corona.

Kadhia hiyo imetokea katika Mji wa Eldoret ambapo wananchi walikuwa wamesimama nje ya nyumba zao wakati amri ya kutokuwa nje ilipoanza na kusema kuwa hawatokubali kukaa majumbani.

Wananchi hao wamesema kuwa hawawezi kukaa ndani kwani inawalazimu wafanyekazi kwa muda mrefu zaidi ili waweze kulisha familia zao, na kwamba muda mzuri kwao wa kufanya biashara ni usiku.

Kenya iliweka sheria ya kutotoka nje wakati wa usiku (dusk-to-dawn curfew) ikiwa ni mkakati wa kudhibiti kuenea zaidi kwa virusi vya corona vinavyosababisha homa ya mapafu. Hadi mapema Machi 30, nchini hiyo imethibitisha kuwepo kwa visa 42 vya waathirika wa COVID-19.