Ofisi mbalimbali za serikali zimelazimika kufungwa leo mjini Hong Kong nchini China, baada ya waandamanaji katika kisiwa hicho kutangaza kuwa na leo wanaendelea na maandamano yao ya kupinga muswada wanaoona kuwa unawanyika demokrasia.
Jana waandamanaji katika jimbo la Hong Kong walipambana na polisi wa kutuliza ghasia, baada ya kuvuka vizuizi vilivyokuwa vimewekwa na Polisi na kuanza kuleta ghasia.
Watu hao wanapinga muswada wa kuwachukua wakazi wa kisiwa cha Hong Kong kwenda bara ya China kushitakiwa. Wanasema hatua hiyo inaondoa maana halisi ya uhuru wao waliougombea, wakitarajia kujitoa kwenye makucha ya wakoloni.