Mwimbaji maarufu duniani Shakira Isabel Mebarak Ripoll maarufu kama ‘Shakira’ na mumewake amabyae pia ni mchezaji wa klabu ya soka ya Barcelona Gerald Piqué wametanga kuvunja ndoa yao iliyodumu kwa miaka 11.
Shakira ambaye amejipatia umaarufu kupitia wimbo wake wa “Hips Don’t Lie” na kisha kibao chake cha waka waka alichokiimba wakati wa kombe la dunia la mwaka 2010 nchini Afrika kusini ameachana na nyota huyo wa Barcelona kwa madai ya kutokuwa mwaminifu.
Wawili hao walioana mwaka 2011 na kubarikiwa watoto wawili, Sasha na Milan.
Katika tamko lao la pamoja wawili hao wamesema “Tunasikitika kuthibitisha kwamba tunaachana. Kwa ajili ya ustawi wa watoto wetu, ambao ni kipaumbele chetu kikubwa, tunaomba muheshimu faragha yao. Shukrani kwa kutuelewa.”