Mwizi wa bumu hadi mhazini wa chuo

0
275

Sibongile Mani amechaguliwa kuwa Mweka Hazina wa kamati ya mikutano ya Chuo Kikuu cha Walter Sisulu (WSU) Eastern Cape, Afrika Kusini, baada ya kupita miaka kadhaa tangu alipohukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa wizi wa fedha za mikopo kwa Wanafunzi.

Mwaka 2018 Mfuko wa Mikopo kwa Wanafunzi Afrika Kusini (NSFAS), ulifanya kosa na kumwekea Mani Rand milioni 14 (takribani shilingi trilioni 1.794) badala ya Rand 1,400 (takribani shilingi 179,400) kama alivyostahili kama mkopo wake wa mwezi.

Mani ambaye kipindi hicho alikuwa ni Mama wa mtoto mmoja, alikutwa na makosa ya matumizi mabaya ya fedha zilizoingizwa kimakosa kwenye akaunti yake na hivyo kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela adhabu aliyoikatia rufaa huku akiendelea kukaa nje.

Ndani ya kipindi cha miezi mitatu, Mani alitumia zaidi ya shilingi milioni 100, kati ya pesa hiyo kwenye mambo ya starehe.