Mwili wa Rais Nkurunziza kuzikwa leo

0
667

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza utazikwa leo kwenye makaburi ya Mji Mkuu wa nchi hiyo, Gitega, uliopo katikati mwa Burundi

Ibada ya mazishi inatarajiwa kuongozwa na Rais wa Burundi, Jenerali Evariste Ndayishimiye na wakuu wengine wa serikali.

Hayati Nkurunziza alifariki dunia Juni, 8 mwaka huu kutokana na shambulio la moyo. Kifo hicho kilitokea ikiwa ni miezi miwili kabla ya kukabidhi madaraka kwa mrithi wake kufuatia uchaguzi uliofanyika Mei 2020.

Kwa mjibu wa tangazo lililotolewa na Serikali ya Burundi, shughuli za mazishi zitaanzia kwenye ‘Hospital du Cenquantenaire Twese Turashoboye’ iliyopo kwenye Mkoa wa Karusi ambako mwili wake umehifadhiwa.

Jeshi litamtolea heshima za mwisho katika Uwanja wa Ingoma mjini Gitega, kabla ya mwili wake kupitishwa mbele ya wananchi watakaokuwa uwanjani humo kumuaga na baadae kufanyika maziko rasmi.