Mwili wa Moi kuwekwa bungeni kesho

0
419

Mwili wa Rais wa Pili wa Kenya, Daniel Arap Moi aliyefariki dunia Jumanne wiki hii,  hapo kesho utapelekwa katika  Bunge la nchi hiyo na kukaa kwa muda wa siku tatu kabla ya kuagwa kitaifa Jumanne Februari 11.

Ukiwa bungeni, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta hapo kesho atawaongoza raia wa nchi hiyo kutoa heshima zao za  mwisho kwa mwili wa kiongozi huyo ambaye ameliongoza Taifa hilo kwa miaka 24 kuanzia mwaka 1978 hadi mwaka 2002.

Jumatano ijayo mwili huo wa Mzee Moi utapelekwa nyumbani kwake Kabarak kwa ajili ya mazishi ya Kitaifa yatakayofanyika kwa heshima zote za kijeshi.