Mwili wa Generali Qasim Soleiman waagwa Iran

0
296

Viongozi wa ngazi za juu nchini Iran, wameaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa majeshi ya nchi hiyo, Qasim Soleiman aliyeuwa na makombora ya majeshi ya Marekani nchini humo, hali iliyosababisha taharuki katika eneo la mashariki ya kati.

Mwili wa generali Soleiman umewasili mjini Tehran, ambapo maelfu ya watu wamejitokeza kuuaga, na baadaye unatarajiwa kupelekwa nyumbani kwao kwa mazishi hapo kesho.

Kifo cha Soleiman kilizusha hasira kwa wapiganaji wa kikundi cha Hizboullah cha nchini Beirut ambao waliahidi kulipiza kisasi licha ya Marekani kutishia kuwa nchi ya Iran ikithubutu kulipiza kisasi maeneo yapatayo 52 ya nchi hiyo yatashambuliwa.

Kiongozi wa kikundi cha Hizboullah alitangaza kuwa askari wote wa Marekani waliopo mashariki ya kati na nchi za kiarabu, pamoja na kambi zao za kijeshi wajiandae kushambuliwa, baada ya kumuua mtu wa muhimu sana katika nchi hizo za kiarabu.