Mwili wa Askofu Tutu waanza kuagwa

0
144

Wananchi wa Afrika Kusini wameanza kuaga mwili wa Mwanaharakati na mpinga ubaguzi wa rangi Askofu Desmond Tutu, aliyefariki dunia nchini humo mapema wiki hii akiwa na umri wa miaka 90 baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Mwili wa Askofu Tutu ambaye ni mshindi wa nishani ya Nobel, umewekwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Georgia mjini Cape Town, ili watu wapate nafasi ya kumuaga kabla ya mazishi yake yanayotarajiwa kufanyika keshokutwa Jumamosi mjini Cape Town.

Askofu Tutu anakumbwa na Wananchi wa Afrika Kusini alivyokuwa akipinga utawala wa kibaguzi wa nchi hiyo uliokuwa ukiongozwa na wazungu, pamoja na vitendo vya ubaguzi wa rangi walivyokuwa wakifanyiwa wazalendo.