Mwandishi wa habari maarufu nchini Philippines matatani

0
643

Mahakama nchini Philippines imemtia hatiani mwandishi wa habari maarufu nchini humo Maria Ressa kwa madai ya kupotosha umma, kwa kuandika taarifa zilizo kinyume na serikali ya nchi hiyo.

Ressa mwenyewe ameendelea kudai kuwa hana hatia na kwamba serikali ya Rais Rodrigo Duterte wa nchi hiyo inajaribu kudidimiza uhuru wa vyombo vya habari nchini humo.

Mwandishi huyo wa habari aliandika katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali ya Philippines.