Mwanamke mwenye dalili zinazofanana na Ebola agundulika Kenya

0
266

Mwanamke mmoja  mwenye dalili zinazofanana na zile za ugonjwa wa Ebola,  anapatiwa matibabu katika kituo kimoja cha afya kilichotengwa kwa ajili ya kupokea watu wenye ugonjwa huo kilichopo katika jimbo la Kericho nchini Kenya.

Sampuli za damu za mgonjwa huyo zimechukuliwa na kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi, ambapo majibu yanatarajiwa kutolewa ndani ya kipindi cha saa 24.

Mwanamke mwenye dalili zinazofanana na Ebola agundulika Kenya

Uongozi wa jimbo hilo la Kericho umesema kuwa, hivi karibuni Mwanamke huyo  alisafiri kwenda katika mji wa Malaba, ambao upo katika mpaka wa Kenya na Uganda.

Tayari watu wawili wamethibitika kufa nchini Uganda baada ya kuugua ugonjwa wa Ebola, ugonjwa ulioanzia kwa mtoto ambaye alisafiri na familia yake kwenda katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo –  DRC na baada ya kurejea nchini humo aligundulika kuwa na virusi vinavyosababisha ugonjwa huo.