Mutharika apinga mahakama kufuta ushindi wake

0
417

Rais Peter Mutharika wa Malawi anakusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama wa kubatilisha ushindi wake katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Mei mwaka 2019.

Februari tatu mwaka huu, mahakama nchini Malawi ilibatilisha ushindi wa Rais Mutharika kwa madai kuwa wakati wa uchaguzi huo taratibu kadhaa zilikiukwa na hivyo kuamuru urudiwe ndani ya kipindi cha siku
150.

Kiongozi wa upinzani nchini Malawi, Lazarus Chakwera amewaambia maelfu ya waandamanaji waliokuwa wakisherehekea uamuzi huo wa mahakama kuwa, hatua hiyo ni ushindi mkubwa kwa demokrasia.

Katika uchaguzi huo Rais Mutharika aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2014 alipata asilimia 38.5 ya kura zote zilizopigwa, huku Chakwera aliyefungua shauri hilo mahakamani akipata kura 35.41 na kushika nafasi ya pili.