Mukwege na Nadia washindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel

0
2286

Denis Mukwege ambaye ni dakatri wa wanawake wa masuala ya uzazi kutoka Jamhuri ya Kidemokarasi ya Kongo na Nadia Murad ambaye ni mwanaharakati kutoka nchini Iraq wametangazwa  kuwa washindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka 2018.

Denis  alipata umaarufu kutokana juhudi zake za kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na kuwahudumia waathirika wa vitendo hivyo, huku Nadia akitambuliwa kuwa ni mmoja wa wanawake takribani elfu tatu kutoka jamii ya Yazidi ambao ni waathiriwa wa vitendo vya udhalilishaji walivyofanyiwa na wanamgambo wa IS wa nchini Iraq.

Tuzo hiyo ya  Amani ya Nobel hutolewa pamoja na zawadi ya zaidi ya dola milioni moja za Kimarekani kwa kila mshindi.

Watu binafsi pamoja na mashirika 331 walipendekezwa kushindania tuzo hiyo Amani ya Nobel kwa mwaka huu, tuzo zilizotangazwa katika mji wa Oslo nchini Canada.