Mtungi wa sumu walipuka na kuua watu 13

0
174

Watu 13 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 250 wamejeruhiwa, baada ya kutokea mlipuko wa mtungu wa hewa ya sumu aina ya chlorine katika bandari ya Aqaba nchini Jordan.

Mlipuko huo umetokea baada ya mtungi huo wa hewa ya sumu uliokuwa na uzito wa tani 25 kudondoka na kulipuka wakati ukipakiwa katika roli kutoka kwenye meli iliyokuwa imebeba shehena ya mizigo.

Katika taarifa yake serikali ya Jordan imeeleza kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Waziri Mkuu wa Jordan, Bisher Al- Khasawneh ametembelea eneo ulipotokea mlipuko huo, kwa lengo la kujionea madhara yaliyotokea.