Kesi ya mtuhumiwa mkuu wa mauaji katika jimbo la Darfur nchini Sudan, – Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman maarufu kama Ali Kushayb kwa mara ya kwanza imeanza kusikilizwa katika mahakama ya Kimataifa ya makosa ya uhalifu wa kivita huko The Hague nchini Uholanzi.
Kesi hiyo imeanza kusikilizwa katika mahakama hiyo baada ya mtuhumiwa huyo kujisalimisha kwa serikali ya Sudan, na baadaye kupelekwa The Hague ili akakabiliane na kesi yake.
Mtu mwingine anayetuhumiwa kuhusika na mauaji katika jimbo hilo la Darfur ni aliyekuwa Rais wa Sudan, – Omar Al Bashir ambaye bado anashikiliwa nchini mwake.