Mtoto wa siku moja akutwa na virusi vya corona

0
317

Mtoto mchanga amebainika kuwa na virusi vya homa ya Corona saa 30 baada ya kuzaliwa mjini Wuhan, China, eneo mlipuko huo ulipoanzia.

Kabla ya mtoto huyo kuzaliwa, mama yake alipimwa na kubainika kuwa na virusi hivyo, lakini matabibu hawajabaini endapo mtoto huyo aliambukizwa virusi vya corona akiwa tumboni au wakati wa kuzaliwa.

Hata hivyo matabibu wengi wanaamini kwamba alipata virusi hivyo akiwa tumboni. Tukio hilo limeamsha muamko kwamba wanatakiwa kuwa makini kuepuka uenezaji wa virusi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

“Lakini pia yawezekana kwamba mtoto huyu alipata virusi baada ya kuzaliwa kutokana na ukaribu aliokuwa na mamaye, mfano kuingiza virusi hivyo kwa njia ya hewa pindi mama anapokohoa,” Stephen Morse, tabibu kutoka Chuo cha Colombia ameeleza.

Shirika la Habari la China, Xinhua, liliripoti kisa hiki cha kipekee Jumatano jioni na kueleza kuwa mtoto huyo aliyezaliwa na 3.25kg amewekwa katika uangalizi maalumu.