Mtoto wa Shah Ruk Khan kizimbani

0
349

Aryan Khan, mtoto wa muigizi maarufu wa Bollywood Shah Ruk Khan, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya.

Aryan mwenye umri wa miaka 23 alikamatwa akiwa kwenye sherehe ambapo polisi baada ya kufanya upekuzi ndani ya meli waliyokuwa wakifanyia starehe pamoja na wenzake saba walimkuta na gramu 13 za ‘cocaine, gramu 21 za bangi, vidonge 22 vya molly na dawa aina ya MD gramu tano.

Mashtaka yanayomkabili Aryan ni pamoja na umiliki, utumiaji na uuzaji wa dawa za kulevya.

Mwanasheria wa Aryan ameomba mteja wake apewe dhamana kwa kuwa hakukutwa na kithibitisho cha kutosha cha yeye kuhusika na dawa hizo..

Katika taarifa yake, kampuni inayomiliki meli ambayo Aryan na wenzake walikuwa wanafanyia sherehe imetoa taarifa kuwa, haihusiki kwa namna yeyote na sakata hilo.