Mswada Tata Hong Kong wafutwa

0
396

Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam amesema muswada tata wa sheria uliozusha mgogoro mkubwa wa kisiasa katika eneo la Hong Kong umefutwa.

Akizungumza na waandishi wa habari kiongozi huyo amekiri kuwa pendekezo la muswada huo lilikuwa ni kosa kubwa lililofanywa na serikali ya Hong Kong na kuwataka raia wake waamini kwamba pendekezo la muswada huo halitojadiliwa tena na hakuna mipango ya kuurejesha mezani.

Siku chache zilizopita Lam alisitisha kwa muda zoezi la kuufanyia marekebisho muswada huo ambao ungewezesha raia wa Hong Kong kupelekwa maeneo mengine ya China kushtakiwa jambo lililozusha maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa mjini Hong Kong.